Home Uncategorized ISHU YA MORRISON YAVUTA HISIA ZA MASHABIKI WENGI

ISHU YA MORRISON YAVUTA HISIA ZA MASHABIKI WENGI


 LEO Agosti 10 Kamati ya Hadhi ya Wachezaji Tanzania inaskiliza kesi ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison ambaye yupo kwenye mvutano na timu yake kuhusu suala la usajili.


Sakata la Morrison limevuta hisia za wengi kutokana na namna mchezaji alivyokuwa na matukio yasiyokwisha kabla ya kutambulishwa na watani za jadi wa Yanga ambao ni Simba.
Suala la kusajiliwa na Simba limeongeza uzito kwa Yanga kuhitaji kupatikana kwa haki jambo ambalo limefanya wengi kufuatilia ili kujua hatma yake itakuaje.

Asubuhi makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) wadau wengi wa masuala ya michezo walijitokeza ili kujua kinachoendelea ambapo wengi waliweka kambi nje ya makao hayo yaliyipo Karume.

Ulinzi umeimarishwa ambapo hakuna anayeruhusiwa kuingia ndani ikiwa hana miadi na kiongozi ndani ya TFF.
SOMA NA HII  SAKATA LA BERNARD MORRISON NA YANGA LAIBULIWA UPYA KABISA