Home Uncategorized ISHU YA SURE BOY KUIBUKIA YANGA IPO HIVI

ISHU YA SURE BOY KUIBUKIA YANGA IPO HIVI


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa iwapo Yanga wanahitaji huduma ya kiungo wao Abubakari Salim maarufu kama Sure Boy wanapaswa wafuate utaratibu uliopo kwa kufika mezani kufanya mazungumzo.
Inaelezwa kuwa Yanga inampigia hesabu Sure Boy ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi chao kwa msimu ujao wa 2020/21 na nyota huyo anatajwa kwenda kuwa mbadala wa Papy Tshishimbi.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit alisema kuwa Sure Boy ni mchezaji muhimu ndani ya Azam FC hivyo ikiwa Yanga kweli wanahitaji huduma yake ni lazima wafuate utaratibu uliopo.
“Nasi pia tunaskia kwamba Yanga wanamhitaji Sure Boy ila ili wampate ni lazima utaratibu ufuatwe kwa kuwa sio rahisi kumpata kiungo ambaye yupo ndani ya kikosi na ana uwezo mkubwa akiwa ni Icon wa timu,” alisema Thabit.
SOMA NA HII  MSUVA AMFUATA SAMATTA ULAYA