Home Uncategorized KUMEKUCHA SIMBA, MAJEMBE HAYA YA KAZI SABA KUIKOSA FAINALI LEO, MMOJA HATMA...

KUMEKUCHA SIMBA, MAJEMBE HAYA YA KAZI SABA KUIKOSA FAINALI LEO, MMOJA HATMA YAKE MIKONONI MWA KOCHA


LEO Uwanja wa Nelson Mandela unatarajiwa kukutana na balaa la wanaume 22 wanaosaka taji la Kombe la FA majira ya saa 9:00 alasiri.

Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck itamenyana na Namungo FC iliyo chini ya Hitimana Thiery.

Haya hapa majembe ya kazi saba ya Simba yanatarajiwa kuukosa mchezo wa leo kwa Simba ni :-
Ibrahim Ajibu, Rashid Juma, Tairone Santos,Sharaf
Shiboub, Haruna Shamte, Shiza Kichuya na Cyprian Kipenye hawa walikosekana
kwenye mechi mbili zilizopita kwa kuwa waliachwa
Dar es Salaam.

Mechi hizo ilikuwa ni mbele ya Coastal Union ya Tanga na ile ya mwisho dhidi ya Polisi Tanzania, Moshi. 

Pascal Wawa raia wa Ivory Coast beki kisiki ndani ya Simba hatma yake ya kuanza mchezo wa leo ipo mikononi mwa Kocha Sven kwa kuwa alionyeshwa kadi mbili za njano  kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union na kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Kwa mujibu wa kanuni alipaswa aukos mchezo mmoja dhidi ya Polisi Tanzania ambao alikuwa mtazamaji hivyo kuanza kwake leo mbele ya Namungo kupo mikononi mwa Sven mwenyewe.

SOMA NA HII  YANGA WANA JAMBO LAO KANDA YA ZIWA