Home Uncategorized YANGA WANA JAMBO LAO KANDA YA ZIWA

YANGA WANA JAMBO LAO KANDA YA ZIWA

KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze kimeendela kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United.


Mchezo huo ambao utakuwa ni wa nane kwa Yanga unatarajiwa kuchezwa Oktoba 30, Uwanja wa Kirumba.


Yanga inakutana na Biashara United ambayo imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania huku wao wakitoka kushinda mabao 2-1 dhidi ya KMC, Uwanja wa CCM Kirumba.


Kipa wao namba moja kwa sasa ndani ya Yanga ni Metacha Mnata wa ambaye amekaa langoni kwenye mechi sita akiwa amekusanya jumla ya clean sheet tano amefungwa bao moja na Hassan Kabunda wa KMC wakati Yanga ikishinda mabao 2-1.


SOMA NA HII  KOCHA TANZANITE: NGUVU ZETU SASA NI KWA AFRIKA KUSINI ILI KUTINGA FAINALI COSAFA