Home Uncategorized KOCHA TANZANITE: NGUVU ZETU SASA NI KWA AFRIKA KUSINI ILI KUTINGA FAINALI...

KOCHA TANZANITE: NGUVU ZETU SASA NI KWA AFRIKA KUSINI ILI KUTINGA FAINALI COSAFA

BAKARI Shime, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Wanawake ‘Tanzanite’ amesema kuwa akili za timu pamoja na wachezaji ni kwenye mchezo wao wa nusu fainali dhidi timu ya Afrika Kusini.

Tanzanite imealikwa kwenye michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini na imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kushinda michezo miwili kwa kuanza ule wa Botswana kwa ushindi wa mabao 2-0 kisha Eswatini mabao 8-0 kabla ya jana kupoteza mbele ya Zambia kwa kufungwa mabao 2-1.

“Mchezo wetu mgumu utakuwa mbele ya Afrika Kusini ambao unakuja na tunajua utakuwa mgumu kama ambavyo ulikuwa mchezo wetu dhidi ya Zambia.

“Tumejipanga na tunapambana kupeperusha Bendera ya Taifa nafasi ipo na kila kitu kinawezekana,” amesema.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here