Home Uncategorized MBWANA SAMATTA AWEKA REKODI HII ENGLAND

MBWANA SAMATTA AWEKA REKODI HII ENGLAND

MBWANA Samatta, mshambuliaji wa Aston Villa ameweka rekodi yake ndani ya Ligi Kuu England baada ya kuibukia huko akitokea Klabu ya KRC Genk kwa kandarasi ya miaka minne.

Samatta raia wa Tanzania ambaye anakipiga pia ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kukipiga Kwenye Ligi pendwa duniani ya Ligi Kuu England.

Amecheza jumla ya mechi 14 ndani ya Premier msimu wa 2019/20 ametupia bao moja na hana pasi ya bao kibindoni.

Amepiga jumla ya pasi 172 wastani wa pasi 12.29 kila mechi huku akipiga jumla ya mashuti 17 na matatu yakilenga lango.

SOMA NA HII  SABABU ZA JKT KUSHINDWA KUTAMBA ZAWEKWA WAZI