Home Uncategorized MIPANGO YA COASTAL UNION KWENYE USAJILI IPO NAMNA HII

MIPANGO YA COASTAL UNION KWENYE USAJILI IPO NAMNA HII

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa mpango mkubwa wa kikosi chake kwa wakati huu wa usajili ni kusajili washambuliaji wazuri ambao watatibu tatizo la timu hiyo.

Mgunda amesema kuwa kwa msimu wa 2019/20 tatizo kwa timu yake lilikuwa upande wa umaliziaji nafasi jambo lililowafanya wasiwe wanapata matokeo kwenye mechi zao za mwisho.

Tayari Coastal Union imewaruhusu wachezaji wake wawili wa kikosi cha kwanza ambao ni Bakari Mwamnyeto beki kwa msimu ujao atakipiga ndani ya Yanga na Ayoub Lyanga kiungo mshambuliaji mwenye mabao nane na pasi nane za mabao msimu ujao atavaa jezi ya Azam FC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mgunda amesema kuwa:”Kwa kikosi kwenye usajili ni muhimu kwetu kusajili washambuliaji kwani hapo ndipo tatizo lilipokuwa.

“Matumaini yetu tutakuwa na kikosi makini ambacho kitatufanya tuwe na kikosi imara kwa msimu ujao,” amesema.

Coastal Union imemaliza ligi ikiwa nafasi ya saba na pointi 53 baada ya kucheza mechi 38.

SOMA NA HII  BALAA LA MWILI JUMBA NDANI YA UWANJA LIPO HIVI