Home Uncategorized NAMUNGO FC WAPAMBANAJI LICHA YA WACHEZAJI WAKE WENGI KUWA WAGONJWA

NAMUNGO FC WAPAMBANAJI LICHA YA WACHEZAJI WAKE WENGI KUWA WAGONJWA

NAMUNGO FC inayonolewa na Kocha Mkuu Hitimana Thiery ni miongoni mwa timu ambazo zimeonyesha ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara hata kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho. 

Licha ya wachezaji wake wengi muhimu kuwa wagonjwa bado aliweza kuonyesha ushindani mbele ya Simba kwenye mchezo wa fainali uliochezwa jana,  Agosti 2 Uwanja wa Nelson Mandela. 

Thiery hakuwa na chaguo baada ya mshambuliaji wake namba moja, Relliants Lusajo mwenye mabao 12 kuwa mgonjwa aliamua kujitoa muhanga kwa kumtumia Edward Manyama. 

Manyama ambaye alitupia bao kwa upande wa Namungo FC naye pia hakuwa fiti asilimia mia kwani naye pia alikuwa ametoka kuugua hivi karibuni.

Thiery amesema:”Nilikuwa na wachezaji wengi wagonjwa ila naona wamepambana na kupata kile ambacho tumepata, bado tuna safari nyingine lazima tuzidi kujipanga. 

“Kucheza na bingwa sio jambo jepesi kwani kila mchezaji wa Simba ni bora na wameonyesha utofauti wao.”

Nurdin Barola kipa wa Namungo FC alikuwa ni nyota wa mchezo kwa kuwa alifanya save moja matata baada ya nahodha wa Simba, John Bocco kuudokoa mpira kidogo kwa juu akiwa eneo sahihi la mpinzani ukakutana na mikono ya Barola aliyeweka lango salama.

Simba ilishinda kwa mabao 2-1 baada ya dakika 90 na kusepa na taji pamoja na hundi ya milioni 50.

Bao pekee la Namungo lilipachikwa na Edward Manyama akiunganisha pasi ya kona ya Abeid Athuman huku yale ya Simba yakifungwa na Luis Miqussone na John Bocco.

SOMA NA HII  MSEBIA ATUA MADEAMA