Home Uncategorized NAMUNGO FC YAMALIZANA NA JEMBE LA KAZI KUTOKA KENYA

NAMUNGO FC YAMALIZANA NA JEMBE LA KAZI KUTOKA KENYA


Amani Kyata, beki wa kati amesaini dili la mwaka mmoja kuitumikia Klabu ya Namungo.


Beki huyo amejiunga na Namungo FC akitokea Klabu ya Kariobangi Sharks ya Kenya leo Agosti 21.

Namungo FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery inakisuka kikosi chake kwa ajili ya kushiriki Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho.

Miongoni mwa wachezaji ambao imemalizana nao ni pamoja na Sixtus Sabilo, Jaffary Mohamed na Fredy Tangalo ambaye alikuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa.
SOMA NA HII  ISHU YA LIGI KUU BARA KUREJEA, SIMBA YATOA TAMKO