Home Uncategorized NYOTA MPYA SIMBA ATUMA UJUMBE HUU KWA BOCCO NA KAGERE

NYOTA MPYA SIMBA ATUMA UJUMBE HUU KWA BOCCO NA KAGERE

 CHARLES Ilanfya, nyota mpya ndani ya Simba kwa msimu wa 2020/21 akitokea KMC amesema kuwa hana hofu na ufalme wa Meddie Kagere na John Bocco ndani ya Simba atapambana kufikia malengo yake.

 

Ilanfya amesaini kandarasi ya miaka miwili kukitumikia kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu Bara atakuwa akipambania namba na washambuliaji wakongwe ndani ya Simba ikiwa ni pamoja na Meddie Kagere aliyetupia mabao 22 na Bocco tisa kwenye ligi kuu msimu uliopita.



Akizungumza na Saleh Jembe, Ilanfya amesema kuwa, anafurahi kukamilisha dili lake la kuibukia Simba kwani ni moja ya hatua kubwa kwake na kwamba hana hofu na wachezaji atakaowakuta zaidi ya kuwaheshimu na kufanya kazi.

 

“Ninajua ninakutana na wachezaji wazuri ndani ya Simba ambayo itashiriki michuano ya kimataifa, sina hofu ila ninawaheshimu nami pia nitapambana kufikia malengo ambayo nimejiwekea pamoja na yale ya timu kiujumla,” amesema.


 Ilanfya akiwa KMC msimu wa 2019/20 amefunga mabao sita ndani ya ligi aliibuka kikosi hapo akitokea Mwadui FC.

SOMA NA HII  KASEKE SHUJAA WA YANGA ACHEKELEA KUCHEZA NA YACOUBA