Home Uncategorized NYOTA WAPYA SIMBA WAANZA MATIZI, MORRISON KAMA KAWAIDA HAISHIWI JAMBO

NYOTA WAPYA SIMBA WAANZA MATIZI, MORRISON KAMA KAWAIDA HAISHIWI JAMBO

 


KIKOSI cha Simba leo Agosti 17 kimeanza maandalizi kwa ajili ya Ligi Kuu Bara pamoja na mechi yao ya siku ya Simba day inayotarajiwa kuchezwa Agosti 23, Uwanja wa Mkapa.


Wachezaji wa Simba wameripoti kambini leo na kuunganisha moja kwa moja mazoezini kwenye uwanja wao uliopo maeneo ya Bunju.


Bernard Morrison kiungo mpya wa Simba ambaye ametokea Klabu ya Yanga alikuwa akionekana ni mwenye furaha huku akicheza  wakati walipokuwa wakienda kambini.


Ameungana na wachezaji wenzake wapya ambao wamesajiliwa kwenye dirisha kubwa lililofunguliwa Agosti Mosi na linatarajiwa kufungwa Agosti 31.

Wachezaji hao ni pamoja na Larry Bwalya, Joash Onyango,Chris Mugalu, Charlse Ilanfya, Ibrahim Ame na David Kameta.

SOMA NA HII  SIMBA YAIPOTEZA JUMLAJUMLA YANGA KWA MKAPA