Home Uncategorized SIMBA WAICHOKONOA YANGA KISA ISHU YA MWANANCHI, DIAMOND ATAJWA

SIMBA WAICHOKONOA YANGA KISA ISHU YA MWANANCHI, DIAMOND ATAJWA

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa watani zao wa jadi Yanga hawataweza kuvunja rekodi waliyoiweka wao kwenye kilele cha Simba day kuanzia perfomance mpaka mkwanja watakaoingiza kwa fedha za kiingilio.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa mipango yao ilikuwa tofauti na wamefanya mambo ambayo ni hatua nyingine kabisa kwenye uwanda wa michezo.

Simba jambo lao walilikamilisha Agosti 22 ambapo ilikuwa ni kilele cha Simba day na walimshusha msanii Diamond kwa Helkopta ndani ya Uwanja wa Mkapa.

Yanga wao jambo lao linafika kilele Agosti 30, Uwanja wa Mkapa nao pia wanamshusha Harmonize kwenye kilele cha Mwananchi jambo ambalo Simba wamesema kuwa hawawezi kufikia walipofika wao.

“Kuanzia kiingilio ilikuwa ni juu na tumeingiza pesa nyingi ambazo wao wengine watashindwa kuivunja. Ikiwa watavunja itakuwa ni maajabu kwa kuwa kiingilio chao wao kinaanzia buku tano sasa watawezaje kutufikia sisi?

“Ishu ya shoo, ujue kumshusha Diamond kwenye jukwaa sio kitu kidogo, Diamond n msanii mkubwa na anapendwa hivyo hebu tusubiri na tuone itakuaje na hiyo Mwananchi day lakini cha msingi ambacho ningewashauri kwanza wahakikishe anakuja kocha kwanza maana ligi inakaribia kuanza,” amesema Manara.


SOMA NA HII  TRY AGAIN AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU KIKAO CHA SIMBA..... ISHU IKO HIVI