Home Uncategorized SIMBA YABAINISHA SABABU ZA KUMFUNGASHIA VIRAGO UCHEBE

SIMBA YABAINISHA SABABU ZA KUMFUNGASHIA VIRAGO UCHEBE

 

UONGOZI wa Simba, umesema kuwa sababu kubwa ya kumtimua Patrick Aussems aliyekuwa kocha wa timu ni suala la fedha pamoja kushindwa kufikia malengo ambayo walikuwa wamejiwekea awali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ukurugenzi ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji,’Mo Dewji’ amesema kuwa Aussems maarufu kama uchebe ni kocha mzuri lakini walishindwana naye kwenye makubaliano.

“Tulitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara tukiwa na Uchebe ni furaha kwetu lakini tulitolewa kwenye Kombe la Shirikisho mapema hatukupenda.


“Ukiachana na hilo baada ya timu kutinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu unaofuata tulishindwa kufika mbali na kupoteza nafasi nne kwa taifa hilo nalo lilituumiza kwani tulishindwa kufikia malengo yetu hilo lipo wazi.

“Vile vigezo vyote alivyokuwa anataka tulitimiza kwani mnajua kwamba kulikuwa na mgogoro kati yake na Masoud Djuma ambaye alikuwa ni kipenzi cha mashabiki, tulipokubaliana kwamba aondoke kwa kuwa malengo yalikuwa ni kuona kwamba uchebe hawi na sababu ya kutuambia kuwa hatukumsikiliza.

“Kwa sasa tupo na Sven Vandenbroeck tunaendelea vizuri kwani ameweza kutwaa taji la Shirikisho na Kombe la Ligi Kuu Bara, hivyo bado tuna malengo makubwa ya kufanya vizuri kimataifa, hatupendi kuishia kwa mataji ya ndani hapana,” amesema.

SOMA NA HII  DUH ORIGI MCHAWI WA MABAO YA USIKU KAMA KAWAIDA, SASA AFIKISHA LA NNE NA KOMBE JUU