Home Uncategorized MASAU BWIRE AJA NA KUPAPASA NA KUKUNG’UTA

MASAU BWIRE AJA NA KUPAPASA NA KUKUNG’UTA


 OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire baada ya kutamba msimu uliopita na msemo wake maarufu ‘mpapaso square’ msimu huu amekuja na msemo mpya 
atakaoutumia msimu wa 2020/21 ambao ni ‘kupapasa na kukung’uta’.

 

Bwire amesema:”Kama ambavyo watanzania wanavyotutambua kuwa sisi ni ‘Barcelona ya Bongo’ hivyo wapinzani wetu wajiandae maana tutawapapasa na kuwakung’uta.

 

“Tumefanya usajili bora wa kikosi chetu na tunajivunia kwa kuwa wachezaji wetu ni wazawa na kocha pia ni mzawa, hatuna presha na msimu huu tutafanya vizuri hiyo ndiyo imani yetu.


“Mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani kila kitu kinakwenda kwa mpangilio mzuri tutatoa burudani kwa mashabiki kama ilivyo falsafa yetu,” amesema.


Kwa sasa, Ruvu Shooting inanolewa na Charles Mkwasa ambaye amekiongoza kikosi hicho kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180.


Mchezo wa kwanza ililazimisha sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Gairo na mchezo wa pili ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Ihefu, Uwanja wa Sokoine. 

SOMA NA HII  MANCHESTER CITY YAIBAMIZA WOLVES NA KUSEPA NA POINTI TATU