Home Uncategorized MITAMBO HII YA MABAO NDANI YA SIMBA YAMPA JEURI SVEN

MITAMBO HII YA MABAO NDANI YA SIMBA YAMPA JEURI SVEN

 


KASI ya ufungaji ya mastraika wawili wa Simba, Chris Mugalu na Meddie Kagere imempa kiburi kocha wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck kwa kusema kuwa inampa nafasi kubwa ya kutamba kwenye Ligi Kuu Bara na hata wakianza kucheza mechi za kimataifa.
Kocha huyo ameongeza kuwa wachezaji wake hao pamoja na wengine wanaocheza eneo la ushambuliaji akiwemo Bernard Morrison wanampa uhakika wa kushinda kwenye mechi yoyote ile kwani nje ya kufunga wanajua kutengeneza nafasi.

 Mugalu na Kagere wote kwa sasa wamefunga mabao mawili kwenye ligi wakiwa sawa na kiungo Mzambia Clatous Chama na Mzamiru Yassin.

 Sven amesema kuwa uwezo huo wa juu wa kufunga wa mastraika wake hao unampa mwanga wa kuona ana uwezo wa kushinda mechi yoyote bila ya kujalisha ni ya ligi au ya kimataifa.

 “Tuna washambuliaji wengi wazuri ambao wanajua kwa kiasi kikubwa kufunga, kitu ambacho ni kizuri kwangu kwa sababu hatutegemei mtu mmoja kwenye hilo.

“Wanacheza kitimu na kupeana nafasi ambazo zinatufanya tuwe na uhakika wa kushinda kwenye mechi yoyote ile iwe ya ligi au kimataifa ambapo tuna miezi michache kabla ya kuanza kupambana,” alimaliza Sven.

SOMA NA HII  KAMA KAWAIDA YAKE, MANARA AMVAA NUGAZ KWA MARA NYINGINE, HIKI NDICHO AMEKIANDIKA