Home Uncategorized MWINYI ZAHERA: KWA MWENDO WA SIMBA, KIMATAIFA HAWAFIKI POPOTE

MWINYI ZAHERA: KWA MWENDO WA SIMBA, KIMATAIFA HAWAFIKI POPOTE

 


MWINYI Zahera, Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi ndani ya Klabu ya Gwambina FC amesema kuwa Simba hawatafika mbali kwenye michuano ya kimataifa ikiwa watacheza kama walivyocheza na wao.


Zahera aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga msimu wa 2018/18 na 2019/20 alipigwa chini kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni timu yake kuboronga michuano ya kimataifa.

Simba, Septemba 26 ilicheza na Gwambina mchezo wa Ligi Kuu Bara na kushinda mabao 3-0 ukiwa ni mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.

Zahera amesema kwa namna ambavyo Simba walicheza hamsini kwa hamsini na kama watacheza hivi kwenye mashindano ya kimataifa hawatafika kokote.


“Nimeona Simba ikicheza ni inacheza vizuri na inapenda kucheza mpira wa pasi, sasa ukiangalia namna ambavyo walicheza na timu yetu ni kwamba tuliweza kwenda nao sambamba mwanzo mwisho licha ya kwamba tumepoteza.

“Wana kazi kubwa ya kufanya kimataifa hasa kwa aina ya mchezo wanaocheza, kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hawatakutana na timu kama hizi za kwetu, kule kuna TP Mazembe wao wanakuja muda wote hawajui habari za pasipasi ni kucheza kwa nguvu mwanzo mwisho.

“Kama mwendo wao utakuwa ni hivi basi itakuwa ngumu kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa kule kunahitaji nguvu nyingi na spidi muda wote ili kushinda.” amesema.
SOMA NA HII  MTAZAME BISHOO NEYMAR, NI ZAIDI YA UMJUAVYO