Home Uncategorized SIMBA; KUTOLEWA MAPEMA LIGI YA MABINGWA NI SOMO KWETU

SIMBA; KUTOLEWA MAPEMA LIGI YA MABINGWA NI SOMO KWETU

 


CLATOUS Chama, kiungo wa Klabu ya Simba raia wa Zambia amesema kuwa kuondolewa kwa timu hiyo msimu uliopita kwenye michuano ya kimataifa ni somo kwao wanaamini watapambana msimu huu kufanya vizuri.


Simba msimu wa 2019/20 iliondolewa kwenye hatua ya awali kwenye michuno ya Ligi ya Mabingwa Afrika, tofauti na msimu wa 2018/19 ilipoweza kuandika rekodi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Chama amesema:-“Nawapongeza viongozi kwa kufanya usajili bora, ukiachana na mashindano mengine tutakayoshiriki, tunafahamu tuna kibarua kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambako kuna ushindani mkubwa.


“Zimebaki siku chache kabla ya kuanza michuano hiyo, naona kila mchezaji hapa anajitahidi kuboresha kiwango chake ili kuingia kwenye kikosi cha kwanza.

“Naamini ubora wa kikosi cha msimu huu na funzo la kuaga mashindano mapema msimu uliopita ni vitu vitakavyotufanya tufanye vizuri. Kikubwa ni sapoti kutoka kwa mashabiki nasi pia tuna amini kwamba tutapambana,” amesema.


Simba kwa sasa ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano. Kinara ni Azam FC mwenye pointi 21 baada ya kucheza mechi 7 na kushinda zote.
SOMA NA HII  KISA BODI YA LIGI, MASAU BWIRE AIGOMEA YANGA ATOA ONYO