UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa upo vizuri kwa msimu wa 2020/21 na utafanya mambo tofauti na msimu uliopita ndani ya ligi kuu bara baada ya kumaliza ikiwa nafasi ya tatu na kukosa kutwaa taji lolote lile.
Oktoba 30 ikiwa Uwanja wa Azam Complex ilikubali sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Tanzania baada ya kutoka kupoteza mchezo wa kwanza mbele ya Mtibwa Sugar kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Jamhuri, Moro.
Ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 9 ikitofautiana idadi ya mabao na Yanga ambayo imefunga mabao 11 huku Azam FC ikiwa imefunga mabao 15.
Zakaria Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa bado wanajambo lao kwa msimu huu wana amini litatimia kwa kuwa safari ya ligi bado inaendelea.
“Bado safari ya ligi inaendelea nasi tuna kazi ya kufanya tunaamini kwamba tutafanya vizuri kwenye kusaka matokeo ndani ya uwanja kwenye mechi zetu zijazo.
“Mashabiki watupe sapoti tutafanya vizuri na hatutawaangusha katika hilo kila kitu kinawezekana kwa kuwa wachezaji wapo vizuri na benchi la ufundi lipo vizuri pia,” amesema.