Home Uncategorized ANAANDIKA HAJI MANARA KUHUSU UBINGWA WA SIMBA

ANAANDIKA HAJI MANARA KUHUSU UBINGWA WA SIMBA


 


Anaandika  Haji Manara Ofisa Habari wa Simba kuhusu namna Simba itakavyoweza kutetea taji la ligi kwa msimu wa 2020/21:-

 
Mwaka juzi tulipoteza na Mbao katika raundi za mwanzo mwanzo za ligi kuu kule Mwanza, nakumbuka hadi chupa za maji tulirushiwa pale kirumba!


Halikadhalika msimu uliopita tulifungwa na Mwadui mwanzoni kabisa mwa msimu, tukaaambiwa tunaachia ubingwa. Mwisho wa msimu tukawa bingwa kwa tofauti ya pointi ambazo ni rekodi ya Tanzania!


Nini maana yangu? Tunakwenda kushinda game ishirini mfululizo za ligi kuu kutokea Jumatatu, after,(baada) ya hizo game tutapiga hesabu zetu vizuri kabisa!


Sure yangu ni kwamba tutakuwa Bingwa wa taifa hili hadi 2028, halafu tutaamua tufanyaje?


Rekodi zinaonyesha kuwa msimu huu Simba impoteza mchezo wake wa kwanza baada ya kucheza mechi tano bila kufungwa.


Ilifungwa bao 1-0 na Tanzania Prisons kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Oktoba 22.


Kwa sasa ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi sita na kesho Oktoba 26 ina kibarua cha kumenyana na Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni.

SOMA NA HII  VIDEO: WAIGIZAJI 10 WALIOFARIKI KABLA YA KUMALIZA MUVI ZAO