Home Uncategorized MEDDIE KAGERE HATIHATI KUIKOSA YANGA NOVEMBA 7

MEDDIE KAGERE HATIHATI KUIKOSA YANGA NOVEMBA 7


 MTUPIAJI namba moja ndani ya Bongo kwa misimu miwili mfululizo akiwa amefunga jumla ya mabao 49 ambapo alifunga mabao 23 msimu wa 2018/19 na mabao 22 msimu wa 2019/20 na mabao manne msimu wa 2020/21 Meddie Kagere kuna hatihati akaukosa mchezo dhidi ya Yanga, Novemba 7 kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Kagere ana zali la kuwafunga Yanga ambapo kwenye mabao yake hayo 49 mawili aliwafunga Yanga, aliwafunga bao moja msimu wa 2018/19 Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikishinda bao 1-0 na kipa alikuwa ni Ramadhan Kabwili na aliwafunga 2019/20 kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 na kipa alikuwa ni Faroukh Shikhalo.

Kwa sasa dabi hiyo ya Kariakoo imebakiza siku 18 na Kagere yupo chini ya uangalizi akitibu majeraha yake aliyoyapata Oktoba 4 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma wakati Simba ikishinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania na yeye alitupia mabao mawili.

 Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kikosi cha Simba kipo vizuri huku kikiwa na wachezaji wachache majeruhi waliopo chini ya uangalizi maalumu.

“Gerson Fraga anaedelea vizuri na John Bocco ameanza mazoezi mepesi. Pia Meddie Kagere ambaye kwa ukweli yeye atakuwa nje kwa muda wa wiki tatu kwa mujibu wa jopo la madaktari mpaka pale hali yake itakapotengemaa atarejea uwanjani.

“Matarajio yetu ni kwamba Wanasimba wataendelea kuwaombea wachezaji wetu ambao ni majeruhi ili warejee kwenye afya zao,” alisema Manara.

Wiki tatu ambazo ni siku 21 zinamfanya Kagere kutokuwa na uhakika wa kuivaa Yanga, Novemba 7 kwa kuwa anaweza kuwa fiti Novemba 6 huku mechi dhidi ya Yanga ni Novemba 7 jambo ambalo linaleta ugumu kwake kuanza kwenye mechi hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

SOMA NA HII  HAKUNA UNYONGE AL AHLY ANAPIGIKA MBONA