Home Uncategorized YANGA KUWAKOSA WATATU LEO, MUANGOLA NAYE HATIHATI,POLISI TANZANIA MMOJA

YANGA KUWAKOSA WATATU LEO, MUANGOLA NAYE HATIHATI,POLISI TANZANIA MMOJA

 


HUENDA kiungo mshambuliaji wa Yanga, Carlos Carlinhos raia wa Angola akaukosa mchezo wa leo Oktoba 22 dhidi ya Polisi Tanzania kwa kuwa anasumbuliwa na majeraha ya enka.


Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa atawakosa wachezaji watatu leo kwenye mchezo wake wa kwanza ambao anatarajiwa kuwa kwenye benchi la ufundi baada ya kusaini dili la miaka miwili akirithi mikoba ya Zlatko Krmpotic.


Wengine ambao wanaweza kuukosa mchezo ni pamoja na Mapinduzi Balama ambaye naye ni majeruhi pamoja na Abdulaziz Makame ambaye alikuwa anaumwa Malaria.


Rekodi zinaonyesha kuwa Carlinhos yeye ni kinara wa pasi za mwisho ndani ya Yanga iliyofunga mabao 7 akiwa nazo mbili na amefunga bao moja.

Mchezo wa leo utachezwa Uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni utakuwa wa kwanza kwa Yanga kwa msimu wa 2020/21 kutumia uwanja huo kwa kuwa mechi zao zilizopita walikuwa wakitumia Uwanja wa Mkapa.

Kwa upande wa Polisi Tanzania watamkosa moja kwa moja mshambuliaji wao Daruesh Saliboko ambaye alionyeshwa kadi nyekundu Kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Gwambina FC.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Amri Abeid ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Msimu uliopita wa 2019/20 walipokutana Yanga na Polisi Tanzania, Uwanja wa Uhuru yalikusanywa mabao sita na hat trick ya kwanza iliandikwa kupitia kwa Ditram Nchimbi zama hizo alikuwa akicheza kwa mkopo Polisi Tanzania akitokea Azam FC.

Timu zote zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 3-3 na kugawana pointi mojamoja.
SOMA NA HII  MOURINHO AMUAGA MMOJA TOTTENHAM