Home Uncategorized KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE U 17 KAZINI LEO COSAFA

KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE U 17 KAZINI LEO COSAFA


Saleh Jembe 

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 17, leo Novemba 4 kinaanza kazi ya kutafuta rekodi ya ubingwa katika michuano ya Cosafa hapa jijini Port Elizabeth, Afrika Kusini.


Vijana hao chini ya Kocha Edna Lema watawavaa Comoro katika mechi itakayopigwa saa 6:30 mchana kwa saa za Afrika Kusini ambazo ni saa 7:30 kwa nyumbani Tanzania.

Tayari michuano hiyo imeanza na Tanzania ni kati ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri.

Kocha Lema amesema wamejiandaa vizuri na wanaamini wataanza na mguu mzuri kwenye mchezo huo.


“Kila kitu sawa na maandalizi yanaendelea vizuri hatuna mashaka kuanzia kwa wachezaji wenyewe namna walivyo sawa.

“Tutaanza na mguu mzuri kwenye mchezo wetu wa leo ambao ni muhimu kwetu,” amesema.
SOMA NA HII  KOCHA ARSENAL AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE