LEO Novemba 5 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea kuchanja mbunga kwa timu sita kusaka pointi tatu uwanjani.
Azam FC ambao wapo nafasi ya pili na pointi 22 wana kazi ya kupambania kombe ili kuona namna gani wanaweza kuwashusha Yanga nafasi ya kwanza wakiwa na pointi zao 23.
Ikiwa leo Azam FC itashinda ama kupata sare mbele ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Azam Complex itaishusha Yanga nafasi ya kwanza kwa kuwa ina wastani wa mabao mengi ya kufunga ikiwa nayo 15 huku Yanga ikiwa imetupia mabao 11.
Mchezo mwingine ni kati ya Mbeya City dhidi ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Mtibwa Sugar itawakaribisha Coastal Union, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.