Home Uncategorized MO DEWJI: UNAMTAKA MIQUISSONE, SUBIRI MIAKA MITATU NA NUSU…

MO DEWJI: UNAMTAKA MIQUISSONE, SUBIRI MIAKA MITATU NA NUSU…

 


Kama kuna klabu ina mpango wa kuingia mkataba na kiungo nyota wa Simba, Luis MIquissone, italazimika kusubiri miaka mingine mitatu na nusu au imwage mamilioni mezani pale Msimbazi.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji amesema mchezaji huyo ana mkataba wa miaka mitatu na nusu na Simba, hivyo hakuna sababu ya kuwa na hofu.


“Kama watahamia kwa Luis, sisi tuko makini sana na tunajua nini tunafanya. Mkataba wake ni miaka mitatu na nusu na hii tunaangalia kwa wachezaji vijana wenye future.


“Sioni kama kuna sababu ya kuwa na hofu, huyu ni mchezaji wetu na vizuri tuendelee na mambo mengine,” alisema.


Dewji amejitokeza mbele ya waandishi wa habari leo na kuzungumzia mambo kadhaa yakiwemo yale waliyojadili katika Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, jana.


Mara kadhaa, kumekuwa na taarifa kwa mchezaji huyo raia wa Msumbiji kuwaniwa na watani wao Yanga.


Taarifa hizo zimekuwa zikieleza kwamba Yanga wanamuwania mchezaji huyo kupitia aliyekuwa CEO wa Simba, Senzo Mbatha na aliapa kuwa atatua Jangwani.


Kauli ya Mo Dewji ainafuta taarifa hizo ambazo zimekuwa zikizagazwa mitandaoni kwa makusudi ili kupeleka taharuki.


SOMA NA HII  LEO UTAKUWA WAPI MAANA MECHI ZOTE KALI ZIPO NAMNA HII, CHEKI RATIBA