Home Uncategorized FA KUMFANYIA UCHUNGUZI CAVAN ISHU YA UBAGUZI WA RANGI

FA KUMFANYIA UCHUNGUZI CAVAN ISHU YA UBAGUZI WA RANGI

 


EDINSON Cavan nyota wa Manchester United anakabiliwa na rungu kutoka Shirikisho la Soka nchini Uingereza (FA) baada ya kuhusishwa na suala la ubaguzi wa rangi kupitia ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii muda mfupi baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Southampton. 


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa St Mary’s,  Cavan alifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao baada ya kuingia kipindi cha pili timu yake ilipokuwa nyuma kwa kufungwa mabao 2-0.


Baada ya kutimiza majukumu yake na kuifanya timu yake kushinda mchezo huo aliandika ujumbe uliosomeka ‘Gracias negrito’ ikiwa inahusiana na ubaguzi ambapo tafsri yake ni ‘ninawashukuru weusi’.


Ujumbe huo ambao aliutuma kupitia mtandao wa twita ulikaa muda wa masaa matatu kisha akaufuta huku akisistiza kuwa neno hilo aliliskia likitumika na watu wa Amerika ya Kusini hivyo hana tatizo ikiwa ataadhibiwa.


FA wanafuatilia juu ya ujumbe huo na anaweza kuchukuliwa hatua ya kufungiwa kucheza mechi pamoja na faini ya fedha.

SOMA NA HII  HUKO SINGIDA UNITED KUMETIBUKA KINOMANOMA, VIONGOZI WAEWA SIKU 7