Home Uncategorized KIDUKU AMTWANGA KWA TKO MTHAILAND

KIDUKU AMTWANGA KWA TKO MTHAILAND


 BONDIA Mtanzania, Twaha Kiduku amemtwanga bondia Sorimongkhon Singwancha kutoka Thailand kwa TKO raundi ya saba.


Kiduku mkazi wa Morogoro aliibuka mbabe kwenye pambano hilo la WBC la uzito wa kilogramu 76 lililofanyika kwenye Ukumbi wa PTA uliopo Sabasaba.


Mthailand huyo alikubali yaishe raundi ya saba baada ya kushushiwa mvua ya makonde ya maana kutoka kwa Kiduku ambaye alionekana kuwa bora mwanzo mwisho.

Mwamuzi, Pendo Njao ambaye naye pia ana uwezo mkubwa kuzichapa akiwa ndani ya ulingo alimaliza pambano hilo raundi ya saba baada ya Mthailand huyo kudai kwamba hataweza kuendelea na balaa uwanjani kwa kuwa alipata maumivu ya bega la kushoto.


Kiduku amesema:”Ninamshukuru Mungu kwa ushindi ambao nimeupata haikuwa kazi rahisi, kujiandaa kwangu na mazoezi ni sehemu ya ushindi wangu.


Mthailand huyo amesema:”Huyu jamaa ni bondia kweli maana anazichapa kwa nguvu mpaka nakubali, nisingeweza kuendelea kupambana kwa kubwa bega langu la kushoto lilipata maumivu makali.”

SOMA NA HII  MBELGIJI WA SIMBA AWAKA KINOMA, AWAPA MAKAVU WACHEZAJI WAKE