Home Uncategorized MARADONA ASHAURIWA KUACHA POMBE

MARADONA ASHAURIWA KUACHA POMBE


LIGENDI wa Argertina, Diego Maradona, ametolewa hospitali siku ya Jumatano, na kuelekea kliniki ya kurekebisha tabia ili kuacha kutegemea pombe.

Nyota huyo ambaye anakumbukwa kwa kufunga bao la mkono, aliliongoza taifa lake katika mashindano ya Kombe la Dunia ya mwaka 1986.

Mapema mwezi huu alifanikiwa kufanya upasuaji katika ubongo ili kuondoa kuganda kwa damu.

 

Wakili wake amesema Diego amepitia kipindi kigumu zaidi katika maisha yake na ilikuwa kama miujiza kukuta damu imeganda katika ubongo wake na angeweza hata kupoteza maisha yake.

 

“Jambo zuri ni kuwa Diego yuko sawa sasa,” alisema wakili wake, Matias Morla, wiki iliyopita.

 

Maradona alilazwa katika kliniki ya Ipensa huko Buenos Aires, akiwa anasumbuliwa na anaemia (upungufu  wa damu).

 

Baada ya upasuaji huo madaktari wamemshauri Maradona kuacha matumizi ya pombe ambayo yanaweza kuchukua uhai wake.

SOMA NA HII  KOCHA MKUU WA BARCELONA SETIEN MAMBO MAGUMU