Home Uncategorized MITAMBO YA MABAO YA SIMBA YAREJEA KIKOSINI

MITAMBO YA MABAO YA SIMBA YAREJEA KIKOSINI

 


MITAMBO ya mabao ndani ya Klabu ya Simba, Meddie Kagere na Luis Miquissone imerejea na kuanza mazoezi pamoja na wachezaji wengine ndani ya kikosi hicho.


Nyota hao wawili hawakuwa sehemu ya kikosi kilichoibuka na ushindi wa mabao 0-7 dhidi ya Coastal Union ya Tanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. 


Luis raia wa Msumbiji na Kagere wa Rwanda walichelewa kujiunga na wachezaji wenzao kwa kuwa walikuwa Kwenye majukumu ya timu zao za Taifa katika harakati za kuwania tiketi ya kufuzu Afcon. 


Simba ikiwa imefunga mabao 29, wawili hawa wamehusika Kwenye mabao 11,Kagere ametupia mabao manne na Luis amefunga bao moja na kutoa pasi sita za mabao.

SOMA NA HII  ZAHERA WA YANGA KUSHUSHA JEMBE MOJA LA KAZI