Home Uncategorized WAWILI WASEPA NA TUZO AFRIKA KUSINI MASHINDANO YA Cosafa

WAWILI WASEPA NA TUZO AFRIKA KUSINI MASHINDANO YA Cosafa


 NYOTA wawili Watanzania ikiwa ni mmoja kutoka Timu ya Taifa ya Tanzania ya U 17 na mmoja kutoka Twiga Stars wameibuka na tuzo mbili nchini Afrika Kusini ambapo Mashindano ya Baraza la Vyama vya Soka Kusini mwa Afrika (Cosafa) yanaendelea.


Miongoni mwa nyota hao ni nahodha wa Timu ya Taifa U 17 Irene Kisisa ambaye ametwaa tuzo hiyo baada ya kuibuka kuwa mchezaji bora wa mchezo dhidi ya Comoros kwenye mashindano ya Cosafa.

Irene anakipiga ndani ya U 17 timu ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Comoros kwenye mchezo wao wa kwanza.

Mwingine ni Kadosho Shaban ambaye naye pia ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo baada ya kutimiza majukumu yake vema kwenye ushindi wa bao 1-0  dhidi ya Zimbabwe, kwenye mchezo uliochezwa Novemba 4.

Kocha Mkuu wa U 17, Edna Lema amesema kuwa ni furaha kwa kuanza na mguu mzuri wana amini wataendelea kupambana ili kupata matokeo zaidi.

SOMA NA HII  KUMBE, HAKUKUWA NA MAELEWAMO MAZURI KATI YA KOCHA ALIYEFUTWA KAZI NA MABOSI WA NAMUNGO