Home Uncategorized ISHU YA VIPIGO VIWILI ILIWAVURUGA KWELI SIMBA

ISHU YA VIPIGO VIWILI ILIWAVURUGA KWELI SIMBA

 


JONAS Mkude, kiungo mkabaji ndani ya Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck, amesema kuwa vipigo viwili walivyopata kwenye mechi zao za ligi kuliwavuruga kwani walijipanga kupata ushindi.

 

Simba imeweka rekodi kwa kuwa timu ya kwanza kupokea vichapo viwili mfululizo kwa timu zilizo ndani ya tatu bora msimu wa 2020/21.


Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 19 na kinara ni Azam FC mwenye pointi 25 na nafasi ya pili ipo mikononi mwa Yanga yenye pointi 23.


Simba ilipoteza mbele ya Tanzania Prisons kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Nelson Mandela, kisha ikapoteza mbele ya Ruvu Shooting kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru.


Mkude amesema kuwa kupoteza mechi zao mbili kuliwavuruga kwa kuwa hawakufikiria ingeweza kutokea hali hiyo.

 

“Kiukweli kuhusu kupoteza mechi mbili mfululizo ndani ya ligi sijui nielezeje maana kulituvuruga, hatukupanga kupoteza ila matokeo ndani ya uwanja yalikuwa yanashangaza, sasa yaliyopita tunaachana nayo tunatazama mechi zetu zijazo,” amesema.


Kesho Simba itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Yanga kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 11:00 jioni.

SOMA NA HII  UHALISIA WA MANARA NA SOKA LA TANZANIA