Home Uncategorized YONDANI ALIPWA NUSU YA FEDHA ZAKE LAKINI ……

YONDANI ALIPWA NUSU YA FEDHA ZAKE LAKINI ……


Wakati Andrew Vincent na Juma Abdul wakiwa wanadai jumla ya milioni 58, beki Kelvin Yondani amelipwa nusu ya fedha zake.

Yondani amelipwa milioni 15 kati ya 25 ambazo alikuwa akidai na sasa amebakiza deni la milioni 10.

Yondani naye ni mmoja wa wachezaji ambao hawakuwa kambini Yanga pamoja na wawili tajwa hapo juu kutokana na kutolipwa fedha hizo.

Mabosi wa Yanga wamekuwa wakipambana kusaka fedha ili kulipa fedha za wachezaji wao ambapo hivi sasa zoezi la kuichangia timu limekuwa likiendelea kupitia kwa wanachama wake.

Hivi sasa Yanga iko katika maandalizi ya kucheza mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ambapo kikosi kimeondoka Dar es Salaam kuelekea nyanda za kaskazini kuweka kambi maalum kuelekea mechi hiyo.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA APEWA MBINU YA KUIMALIZA FC PLATINUM LEO