Home Uncategorized WAWILI WADAI MILIONI 58 YANGA

WAWILI WADAI MILIONI 58 YANGA


Taarifa zinaeleza kwamba uongozi wa Yanga bado unapambana kulipa madeni ya wachezaji wao kadhaa ambao bado wanaidai klabu hiyo yenye masikani yake mitaa ya Twiga iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam.


Wachezaji wanaodai fedha hizo ni Kelvin Yondani, Juma Abdul na Andrew Vincent maarufu kama Dante aliyejiunga Yanga akitokea Mtibwa Sugar.

Taarifa zilizopo ni kuwa Juma Abdul anaidai Yanga jumla ya milioni 40 ambazo ni shilingi za kitanzania huku Dante akidai milioni 18 ambazo jumla ni milioni 58.

Ikumbukwe wachezaji hao waliondoka kambini kufuatia madai ya fedha hizo huku uongozi ukishindwa kuliweka wazi suala lao juu ya madai hayo.

Wakati wawili hao wakiwa wanadai, Yanga hii leo imeondoka jijini Dar es Salaam kuelekea nyanda za juu kaskazini ili kujiandaa na mechi ya mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga itacheza mechi hiyo na Township Rollers huko Botswana Agosti 23 baada ya mtanange wa awali uliopigwa Jumamosi iliyopita jijini Dar es Salaam kumalizika kwa sare ya 1-1.
SOMA NA HII  ILI KUKABILIANA NA KUNDI D GAMONDI AITUMIA LIGI KUU