Home Uncategorized YANGA YATAJA MITAMBO YA USHINDI DHIDI YA NAMUNGO

YANGA YATAJA MITAMBO YA USHINDI DHIDI YA NAMUNGO

 


CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa viungo wake kwa sasa wameshikilia ushindi kwenye mechi zake zote atakazoingia uwanjani ikiwa ni pamoja na mchezo dhidi ya Namungo utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, kesho Novemba 22.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kaze amesema kuwa wachezaji wake wengi kwa sasa wamekuwa bora jambo ambalo anaamini kuwa watampa matokeo mazuri ndani ya uwanja kwenye mechi zake.

Kaze amemtaja kiungo wake Farid Mussa mwenye pasi mbili za mabao na Carlos Carlinhos mwenye pasi mbili na bao moja kati ya 12 yaliyofungwa na kikosi hicho kwenye mechi 10.

“Ni mbinu kwenye kila mchezo kusaka pointi tatu na kupata mabao mengi ila tumekuwa tukishindwa kufanya hivyo kwa kuwa wachezaji wangu wengi mbinu yao ni moja ya kutokea pembeni.

“Nimewaambia viungo wangu wote ikiwa ni pamoja na Fard,(Mussa), Carlinhos (Carlos) kwamba wanatakiwa wabadilishe mbinu, wasitegemee mipira ya kutoka pembeni bali wanatakiwa wawe watulivu na mbinu nyingine ambazo nimewapa siwezi kuziweka wazi,” amesema Kaze. 

SOMA NA HII  WAZIRI ZUNGU MGENI RASMI SWAHILI CUP