Home Uncategorized MRITHI WA FRAGA APEWA MAJUKUMU MAZITO

MRITHI WA FRAGA APEWA MAJUKUMU MAZITO


 KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa ujio wa kiungo mpya Taddeo Lwanga ndani ya timu hiyo utaongeza uimara katika safu yake ya kiungo ambayo anaamini ndio mwanzo wa mafanikio kwa timu yake haswa katika michuano ya kimataifa.

 

Taddeo mwenye uraia wa Uganda, Jumatatu, Desemba 7 alianza rasmi kufanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Simba ikiwa ni siku chache tangu asajiliwe na timu hiyo na alionekana kuyateka mazoezi hayo kutokana na jinsi alivyoonyesha uwezo mkubwa wa kukaba na kutoa pasi.

  

Kocha huyo amesema kuwa ujio wa mchezaji huyo utaongeza uimara katika kikosi chake haswa ukizingatia ushiriki wa timu hiyo katika michuano ya kimataifa, kutokana na ubora wake katika kukaba na kutibua mipango ya wapinzani.


“Lwanga ni moja kati ya viungo bora katika idara ya ukabaji, ni mzuri kwenye kutibua mipango ya maadui bila kusahau uwezo wake wa kuokoa ile mipira ya juu ambayo imekuwa ni shida kwetu wakati mwingine, baada ya ujio wake naamini ataongeza kitu katika kikosi chetu.

 

“Katika michuano ya kimataifa ili uweze kusonga mbele unahitaji wachezaji wa kila aina ili uweze kufanikiwa, katika eneo la kiungo tulihitaji mtu wa aina yake tunashukuru kuwa naye kwani tuna malengo makubwa ili kukamilisha ndoto zetu,” amesema kocha huyo.


Akiwa amesaini dili la miaka miwili ndani ya Simba amekabidhiwa jezi namba nne ambayo ilikuwa inavaliwa na Gerson Fraga ambaye ni raia wa Brazili.


Kwa sasa nyota huyo anaendelea kujitibia jeraha lake la mguu baada ya kuumia Uwanja wa Mkapa wakati alipokuwa akicheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United.

 

SOMA NA HII  KOCHA YANGA ATAJA SIKU YA KURUDI BONGO