Home Uncategorized NYOTA NGORONGORO HEROES KUWAKOSA SAUDI ARABIA

NYOTA NGORONGORO HEROES KUWAKOSA SAUDI ARABIA


KHELFFIN Salum Hamdoun, nyota wa timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes ataukosa mchezo wa leo dhidi ya Saudi Arabia baada ya kuvunjika kidole akiwa mazoezini. 


Saudi Arabia imeomba mechi ya marudiano na Ngorongoro Heroes baada ya ule wa kwanza uliochezwa hivi karibuni kushuhudia ikimaliza dakika 90 ikiwa imefungwa bao 1-0.

Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Jamhuri Kihwelo, ‘Julio’ amesema kuwa ni mchezaji mmoja ambaye atakosekana kwenye mchezo wa leo.

“Fini ameumia kidole alipokuwa mazoezini hivyo ataukosa mchezo wa leo dhidi ya Saudi Arabia ambao ni wa marudio.

“Aliumia wakati akigombea mpira na mwenzake kwenye mazoezi hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza lakini anaendelea vizuri,” amesema.

SOMA NA HII  NAMUNGO WANACHOKITAFUTA NI HIKI HAPA