Home Uncategorized SIMBA KUSHUSHA MTAMBO HUU MABAO KUTOKA CONGO

SIMBA KUSHUSHA MTAMBO HUU MABAO KUTOKA CONGO


 MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, ameahidi kutumia zaidi ya Sh milioni 500 ili amshushe straika mpachika mabao atakayeingia moja kwa moja kikosi cha kwanza ambapo ametajwa kuwa ni staa wa Orlando Pirates, Jean Makusu, na imeelezwa kuwa wapo kwenye hatua nzuri.

 

Pamoja na Makusu kuwa kwenye mkataba na timu ya RS Berkane ya nchini Morocco akiwa anaichezea Orlando kwa mkopo, bado Mo amevutiwa naye japo dau lake likitajwa kufi kia Sh milioni 800, ambazo Mo amekubali kutoa nusu au robo tatu ya kiasi hicho cha fedha.


Mkataba wa Makusu unatarajiwa kufikia ukingoni Juni, mwakani, hii ni kwa taarifa ya umiliki wake ambayo ni Kampuni ya Bro Management ambayo ina wamiliki pia wachezaji wengine wa Ligi Kuu Bara, Mukoko Tonombe wa Yanga na Clatous Chama wa Simba.

 

Chanzo kimeeleza kuwa Simba ilikuwa kwenye mazungumzo na kiungo wa Plateau United ya Nigeria, Oche Ochewechi, ila wamebadili kwanza baada ya kuona mahitaji makubwa upande wa safu ya ufungaji kuelekea kwenye michuano ya kimataifa ambayo lengo lao la kwanza ni kufika hatua ya nusu fainali.


Kwenye dirisha hili dogo, sisi malengo yetu yalikuwa ni kuongeza beki na kiungo mkabaji na hili lilikuja baada ya kumsajili Chris Mugalu, ila kadiri muda unavyosonga mbele tunaona mahitaji ya ufungaji nayo yanakuwa makubwa na hili ameliona zaidi mwenyekiti wetu wa bodi, Mo.


Kufuatia hali hiyo sasa amelazimika kufuatilia uwezo wa kushushiwa gharama ya Makusu ili tuone kama ataweza kuendana na gharama inayotajwa kisha tuingie mezani na wamiliki wake kwani tayari tulishafanya mazungumzo ya kina na nyota mwingine wa Plateau United ambaye tumesimama kidogo ili tuone uwezekano wa kumpata Makusu,” kilisema chanzo hicho.


Chanzo:Championi

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURAAA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO