Home Uncategorized BOSI WA AZAM FC KUKUTANA NA MWANAFUNZI WAKE WA ZAMANI LEO

BOSI WA AZAM FC KUKUTANA NA MWANAFUNZI WAKE WA ZAMANI LEO


 KELVIN Yondani, ingizo jipya ndani ya kikosi cha Polisi Tanzania leo anatarajiwa kuanza kazi dhidi ya bosi wake wa zamani kwenye benchi la ufundi George Lwandamina ambaye anaifundisha Azam FC.

 

Lwandamina mwenye miaka 57 raia wa Zambia, alimfundisha Yondani alipokuwa kocha wa Yanga msimu wa 2016/18.


 Leo anakutana na mwanafunzi wake wa zamani akiwa kwenye maskani mpya ya kucheza huku naye pia akiwa kwenye kibarua kipya cha kufundisha.


Yondani amejiunga na Polisi Tanzania kwa dili la mwaka mmoja akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na timu yake ya Yanga kumeguka msimu wa 2019/20 na hakuongeza mkataba mwingine.

 

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kuwa taratibu zote kuhusu usajili wa Yondani zimekamilika.


“Uongozi umekamilisha kila kitu kuhusu mchezaji wetu Yondani hivyo kwa sasa ni kazi ya benchi la ufundi kuamua kama atamtumia ama la, ila sisi hatuna tatizo naye,” amesema Lukwaro.


Huu unakuwa mchezo wa kwanza kwa Azam FC wa mzunguko wa pili msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara.


Walipokutana Uwanja wa Azam Complex, Azam FC ilishinda bao 1-0 na kubakiza pointi tatu Bongo, leo watakuwa Uwanja wa Ushirika.

SOMA NA HII  KISINDA KUFANYIWA VIPIMO ZAIDI ILI KUPATA MATIBABU