Home Uncategorized BENCHI LA UFUNDI SIMBA LAFANYA ZIARA UWANJA WATAKAOSAKA USHINDI JUMATANO

BENCHI LA UFUNDI SIMBA LAFANYA ZIARA UWANJA WATAKAOSAKA USHINDI JUMATANO

 


BENCHI la ufundi la Klabu ya Simba, leo Desemba 20 wamekagua Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe ambao utatumika Septemba 23 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.


Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji na msaidizi wake Seleman Matola ambaye ni mzawa kimeshapiga kambi nchini Zimbabwe.

Desemba 18 kiliwasili nchini humo ikiwa ni hesabu za Sven katika kutaka kikosi kiweze kuzoea mazingira ya ugenini.

Kocha huyo ameweka wazi kwamba wana kazi kubwa ya kufanya ugenini ili kusaka ushindi kwa kuwa lengo ni moja kushinda ili kutinga hatua ya makundi.
“Malengo yetu ni kuona kwamba tunashinda na kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa kwanza kisha ule wa marudio nao tutapambana kusaka ushindi.

“Wapinzani wetu ni timu kubwa na imara ila haitupi mashaka kwa kuwa nasi pia tupo imara,” .
SOMA NA HII  CHOZI LA SUAREZ KWA FC BARCELONA LIMEZALIWA HAPA