Home Uncategorized BERNARD MORRISON:TUTAPAMBANA KUFIKA MBALI KIMATAIFA

BERNARD MORRISON:TUTAPAMBANA KUFIKA MBALI KIMATAIFA


 NYOTA Simba, Bernard Morrison amesema kuwa wanaamini watapambana kufika mbali kimataifa ili kuwapa furaha mashabiki na kutimiza malengo ambayo wamejiwekea.


Simba imetinga hatua ya mtoano Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuing’oa Plateau United Kwenye mechi za hatua ya awali.


Mchezo uliowapa nafasi ya kupeta mazima ulikuwa ni wa ugenini uliochezwa Novemba 29 ambapo Simba ilishinda bao 1-0  Uwanja wa New Jos lilipachikwa na Clatous Chama kwa pasi ya Luis Miquissone. 


Mchezo wa pili uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Desemba 5,Simba ililazimisha sare ya bila kufungana na kufanya ishinde hatua inayofuata ambayo ni ya mtoano.


Morrison amesema:”Ninaona kwamba mashabiki wanafurahi kuona tunasonga mbele hata sisi pia tunafuraha, kikubwa ambacho tunakwenda kukifanya ni kuongeza juhudi kwa ajili ya mechi zetu zijazo.


“Malengo yetu ni kuona tunafika mbali na hili linawezekana ikiwa kila mmoja anatimiza wajibu wake na ndicho tunachokwenda kukifanya,” amesema. 


Mchezo ujao wa hatua ya mtoano kwa Simba ni dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe. 


SOMA NA HII  SIMBA YATUMA UJUMBE WA KIBABE KWA NAMUNGO FC