Home Uncategorized BIASHARA UNITED KUBORESHA KIKOSI CHAKE DIRISHA DOGO

BIASHARA UNITED KUBORESHA KIKOSI CHAKE DIRISHA DOGO


 FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United amesema kuwa atafanya maboresho kwenye kikosi hicho kwenye dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufunguliwa Desemba 15.


Biashara United yenye maskani yake Mara na inatumia Uwanja wa Karume ipo nafasi ya 7 ikiwa imekusanya pointi 20 baada ya kucheza mechi 14.


Akizungumza na Saleh Jembe, Baraza amesema kuwa wanaamini kwamba ili wawe bora ni lazima kufanya maboresho kwenye kikosi hicho.


“Tunavijana wengi ambao wanajituma na kufanya kazi bila kukata tamaa sasa nina amini kwamba tukiboresha kidogo pale kwenye mapungufu tutakuwa imara zaidi.


“Ninadhani sehemu ya ushambuliaji ni muhimu zaidi pamoja na ulinzi kwa kuwa tumekuwa tukitengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia, tusubiri na tuone dirisha likifunguliwa tutajua itakuaje,” amesema.


Safu ya ushambuliaji ya Biashara United imefunga mabao nane na kinara ni Kelvin Friday mwenye mabao mawili huku ile ya ulinzi imeruhusu mabao 14.


Kipa wake namba moja ambaye anamuamini ni mzawa Daniel Mgore ambaye amekuwa imara akiwa ndani ya lango.

SOMA NA HII  METACHA AREJEA KIKOSINI YANGA