Home Uncategorized DAVID KISSU: BADO TUPO IMARA, TUTAREJEA KWENYE UBORA

DAVID KISSU: BADO TUPO IMARA, TUTAREJEA KWENYE UBORA


 DAVID Kissu, kipa namba moja wa Azam FC amesema kuwa bado timu yake ina nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zinazofuata licha ya kukosa matokeo mazuri.


Jana Novemba 30, Azam FC ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Biashara United mchezo uliochezwa Uwanja wa Karume.


Kissu alitunguliwa bao dakika ya 58 kwa shuti kali nje ya 18 lililopigwa na Timothy Bolton raia wa Kenya ambaye alikuwa msumbufu kwenye mchezo huo.


Kipa huyo ambeye ameanza langoni kwenye mechi zote 13 ambazo Azam FC imeshuka uwanjani amefungwa jumla ya mabao 7 kwa msimu wa 2020/21.


Nyota huyo amesema:”Bado tuna nafasi ya kuendelea kufanya vizuri ndani ya ligi, haya ni matokeo ambayo yanapatikana ndani ya uwanja na kila timu inahitaji ushindi kama ambavyo nasi tunahitaji pia.


“Ukweli ni kwamba pale ambapo tunashindwa kupata ushindi huwa tunaumia lakini hakuna chaguo zaidi ya kupambana kwa mechi ijayo ile ambayo imepita hatuna namna ya kubadili matokeo,” .


Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 26 kibindoni mchezo wake ujao ni dhidi ya Gwambina FC Uwanja wa Gwambina Complex.

SOMA NA HII  SIBOMANA ATOA KAULI YA KUTISHA YANGA