Home Uncategorized HAJI MANARA AFUNGUKIA HATMA YAKE YA KUSEPA SIMBA

HAJI MANARA AFUNGUKIA HATMA YAKE YA KUSEPA SIMBA

[the_ad id="25893"]


 OFISA Habari wa Simba , Haji Manara amesema kuwa bado atabaki kuwa ndani ya Simba kuendelea na majukumu yake licha ya habari kueleza kuwa amesimamishwa na mabosi zake.

Hivi karibuni ilikuwa ikielezwa kwamba Manara amesimamishwa ndani ya Simba jambo ambalo limemfanya asizungumze masuala ya timu hiyo jambo ambao alilikanusha kwa kusema kwamba alipewa mapumziko na uongozi baada ya kufunga ndoa.


Kupitia ukurasa wake wa Intagram, Manara amesema:-“Huu ukubwa wa jina langu unaniponza, umaarufu wangu unawaumiza wengine.

“Sikuwahi kutaka kuwa hivi, lakini kazi yangu naamini imewavutia wengi na Mungu akaamua kunipandisha.

“Please Please Please (Tafadhali) Wanasimba mimi Haji wenu bado nipo nanyi na nitaendelea kuwa msemaji wenu hadi pale riziki yangu itakapokwisha, ( Hatatokea mmoja wetu kubaki milele iwe kwa kifo au vinginevyo )

Waambieni wenye kuandika tetesi za kuondoka kwangu, mimi mtu dhaifu lakini ni mjuzi mno katika mambo ya mawasiliano ya umma na nina uzoefu mkubwa katika eneo hili na nishakuwa sugu na changamoto za kazi.

“Halafu waulizeni Simba namuachia nani ?

SOMA NA HII  NINJA AKUTANA NA ZLATAN LA GALAXY

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here