Home Uncategorized IHEFU V YANGA LEO NI BALAA NDANI YA UWANJA

IHEFU V YANGA LEO NI BALAA NDANI YA UWANJA


 LEO, Uwanja wa Sokoine kutakuwa na vita ya kusaka pointi tatu kati ya Ihefu FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila na Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

Mchezo wa leo ndani ya uwanja ni balaa la kuweka mbali na watoto kwa sababu kila timu imekuwa na matokeo chanya kwenye mechi  mbili mfululizo jambo litakaloongeza ushindani katika kulinda rekodi zao.

Mechi mbili, Ihefu imeshinda kwenye mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar kwa mabao 2-1 na mchezo wa pili ilishinda bao 1-0 dhidi ya KMC inakutana na Yanga ambayo imetoka kushinda mabao 5-0 dhidi ya Mwadui FC na imeshinda mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji.

Unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu hizi kukutana ndani ya uwanja kwenye Ligi Kuu Bara kwa kuwa Ihefu imepanda msimu huu kutoka Ligi Daraja la Kwanza baada ya kushinda mchezo wa play off dhidi ya Mbao FC.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 40 inakutana  na Ihefu ambayo ipo nafasi ya 16 na pointi zake 13 zote zikiwa zimecheza jumla ya mechi 16.

Kocha Mkuu wa Ihefu, Zuber Katwila ameliambia Spoti Xtra kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani na wanatambua kwamba utakuwa ni mchezo mgumu.


Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze ameliambia Spoti Xtra kikosi kipo kamili watatoa burudani kwa mashabiki.

SOMA NA HII  MATOLA: AKIPATIKANA MDHAMINI MKUU, MSIMU UJAO UTANOGA