Home Uncategorized KICHUYA ATUMA UJUMBE HUU KWA MASHABIKI WAKE

KICHUYA ATUMA UJUMBE HUU KWA MASHABIKI WAKE


 SHIZA Kichuya nyota wa Klabu ya Namungo FC inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika amesema kuwa ana imani ya kurejea kwenye ubora wake wa zamani ambao wengi walikuwa wanautambua.


Kichuya alipata kuwika alipokuwa ndani ya Simba na alipata zali la kucheza soka la kulipwa nchini Misri kwenye Klabu ya Pharco ambapo huko alikutana na ugumu wa kupata namba kikosi cha kwanza.

Alirejea ndani ya Simba msimu wa 2019/20 na kufunga bao moja mbele ya Ruvu Shooting, kwenye sare ya kufungana bao 1-1. Maisha yake pia hayakuwa na furaha kwa kuwa hakuwa na namba kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck.


Kwa sasa yupo zake Namungo akiendelea kupambana katika kutimiza majukumu yake n Hivi karibuni alikuwa kwenye sakata la kufungiwa na Fifa kutokana na kile kilichoelezwa kwamba kukiuka masharti ya mkataba wa timu yake ya zamani ya Misri.

Ila kwa sasa ameruhusiwa kuendelea na shughuli za mpira baada ya washtakiwa Simba, kukata rufaa kupinga shauri hilo.

Kichuya amesema:”Bado mapambano yanaendelea kwani ukiwa mchezaji kazi yako ni kuonekana ndani ya uwanja na kufanya kile ambacho kitakuwa na matokeo mazuri.


“Kwa sasa bado tupo imara na imani yangu ni kuona kwamba timu inafanya vizuri nasi tunapata matokeo chanya hakuna kingine.

“Mashabiki wazidi kutupa sapoti nasi pia hatutawaangusha kwenye kazi ambayo tunaifanya,” .

Kesho Namungo itakuwa na kibarua cha kusaka ushidni kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ikiwa ni hatua ya tatu.

Itakutana na Green Warriors, mchezo utachezwa Uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  HUKU UNITED IKIMPIGA MTU 4-0, RASHFORD NA POGBA WACHEZAJI BORA WA MECHI