Home Uncategorized NYOTA MPYA YANGA:UZOEFU UTANIBEBA

NYOTA MPYA YANGA:UZOEFU UTANIBEBA


 NYOTA mpya wa Klabu ya Yanga kiungo mshambuliaji Said Ntibanzokinza amesema kuwa ana amini kuwa anaweza kufanya vizuri ndani ya Ligi kwa kuwa ana uwezo wa kufanya vizuri.


Nyota huyo ambaye ni ingizo jipya kwenye dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufunguliwa Desemba 15 tayari ameshaanza mazoezi na wachezaji wenzake baada ya kutua Bongo Desemba 2.


Amesaini dili la miaka miwili akiwa ni mchezaji huru ila alikuwa anafanya mazoezi na timu yake ya zamani ya Vital’O ya Burundi na amefanya vizuri kwenye timu ya taifa ya Burundi kwa kufunga mabao matatu muhimu kwenye mashindano ya kimataifa.


Akizungumza na Saleh Jembe, Said amesema kuwa uzoefu wa kucheza ligi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulaya ni sababu inayomfanya aamini kwamba hatafanya vibaya kwenye ligi ya Bongo.

“Nina amini kwamba uzoefu ambao ninao kwenye ligi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kucheza ulaya kwangu ni faida na itanipa nguvu ya kufanya vizuri.


“Ninatambua kwamba ushindani ni mkubwa nami nipo tayari, ikiwa timu inaongoza ligi na inashinda mechi zake maana yake ipo vizuri nami nitapambana kuwa vizuri,” amesema.


Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza mechi 14 kesho itakuwa na kibarua cha kucheza na Mwadui FC kwenye mchezo wa ligi.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA AHOFIA REKODI ZA TANZANIA PRISONS