Home Uncategorized INGIZO JIPYA NDANI YA SIMBA KUIBUKIA COASTAL UNION

INGIZO JIPYA NDANI YA SIMBA KUIBUKIA COASTAL UNION


INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Simba Charles Ilanfya huenda akatolewa kwa mkopo kwenda ndani ya Klabu ya Coastal Union baada ya mabosi wake wa zamani KMC kumchunia.


Nyota huyo ambaye ni chaguo la Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kwenye usajili wa msimu wa 2020/21 amekuwa hana nafasi ndani ya kikosi hicho kwenye kikosi cha kwanza.

Ugumu wa namba amekuwa akiupata kutokana na uwepo wa John Bocco na Meddie Kagere ambao ni chaguo la kwanza la Sven huku Chris Mugalu naye pia akiwa ni chaguo la raia huyo wa Ubelgiji.
Ilanfya aliomba kuibukia ndani ya KMC ambapo alikuwa msimu wa 2019/20 ila mabosi wake wamekaa kimya kujibu dili hilo jambo linalomfaya kwa sasa afikirie kwenda Coastal Union.
Ndani ya Ligi Kuu Bara, mshambuliaji huyo mzawa amecheza mechi moja ilikuwa ni mbele ya Tanzania Prisons ambapo alitumia dakika 62 pekee.
Akizungumza na Saleh Jembe kuhusu ishu hiyo nyota huyo amesema:”Bado sijaambiwa chochote kwa sasa,” .

Habari zinaeleza kuwa nyota huyo yupo kwenye mpango wa kutolewa kwa mkopo ili akapate changamoto mpya na timu inayopewa nafasi kumpata ni Coastal Union.
SOMA NA HII  VIDEO; UFAFANUZI JUU YA ISHU YA TIKETI KWA YANGA ZILE ZA MWANCHI HUU HAPA, MASHABIKI WAITWA UWANJA WA TAIFA