MAURICIO Pochettino, Kocha Mkuu wa Klabu ya Paris Sait-Germain, (PSG) anahitaji saini ya kiungo Christian Eriksen ambaye alifanya naye kazi zama zile alipokuwa ndani ya kikosi cha Tottenham.
Kocha huyo ambaye alikuwa ndani ya Tottenham kabla ya kufutwa kazi kutokana na matokeo mabovu ndani ya timu hiyo ambayo kwa sasa ipo mikononi mwa Kocha Mkuu, Jose Mourinho anahitaji kuboresha kikosi hicho kwa kusajili wachezaji anaoamini watampa matokeo chanya.
Mbali na nyota huyo pia anahitaji kumchukua kwa mkopo Delle Alli na hawa wote alifanya nao kazi kwa ukaribu kabla ya kufukuzwa ndani ya Spurs.
Taarifa zinaeleza kuwa chaguo la kwanza kwa Pochettino ni Eriksen ambaye kwa sasa yupo zake ndani ya Inter Milan huku akiwa hana nafasi kikosi cha kwanza kwa kuwa amecheza jumla ya mechi 25 na ametupia bao moja.
Alidumu ndani ya Spurs kuanzia msimu wa 2013-2020 ambapo alicheza jumla ya mechi 226 na alitupia mabao 51.