Home Uncategorized RASTA STARS ANAYEWINDWA NA YANGA AKUBALI KUSAINI SIMBA

RASTA STARS ANAYEWINDWA NA YANGA AKUBALI KUSAINI SIMBA


 ADAM Adam, nyota wa Klabu ya JKT Tanzania ambaye jina lake lipo kwenye orodha ya nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachojiandaa na michuano ya CHAN amesema kuwa atasaini Simba ikiwa watampa dili lenye maslahi mazuri.

Adam mwenye mabao saba ndani ya Ligi Kuu Bara na pasi moja ya bao amekuwa akitajwa kuhitajika ndani ya Klabu ya Yanga ambayo ilianza kumpigia hesabu pamoja na Simba zote zenye makazi yao pale Kariakoo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Adam mwenye rasta kichwani amesema kuwa amepata ofa nyingi ndani ya ardhi ya Bongo pamoja na nje jambo analosubiri ni kuona wapi kutakuwa na ofa kubwa.

“Kwa Bongo timu kubwa zimekuwa zikinifuata na zinahihitaji kupata saini yangu. Kwangu mimi sina tatizo hata Simba ninasaini ikiwa tu wataweka ofa nzuri ambayo itakuwa na maslahi kwangu.

“Kikubwa kwa mchezaji ni kuona anapata nafasi ya kupata changamoto mpya na ninaamini katika uwezo wangu ninaweza kufanya vizuri zaidi hivyo ni suala la muda tu.


“Kuwa ndani ya Stars pia kunanifanya nizidi kuongeza juhudi ili niwe bora kwani hakuna ambaye anapenda kuitumikia timu yake ya taifa hilo lipo wazi kwa kila mchezaji,” amesema.


Januari 10, Stars inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Congo, Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  DILI LA SIMBA NA MSHAMBULIAJI MGHANA WA ASANTE KOTOKO LIMEISHA KWA MTINDO HUU