Uncategorized

YANGA WAJIPANGE KUVUNJA BENKI KUMPATA CLATOUS CHAMA WA SIMBA

admin January 10, 2021 3:47 am


IKIWA mabosi wa Yanga bado wapo kwenye hesabu za kupata saini ya nyota wa Simba, Clatous Chama inabidi wajipange kuvunja benki kuipata saini ya nyota huyo.

Awali ilikuwa inaelezwa kuwa mwamba huyo mwenye tuzo ya mchezaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/21 yupo kwenye rada za watani hao wa jadi.


Msimu wa 2019/20 alifunga mabao mawili ndani ya Simba na kutoa pasi 10 za mabao pia jina lake lilikuwa kwenye orodha ya kikosi bora  na tuzo nyingine aliyosepa nayo ni ile ya kiungo bora.

Tayari Chama ambaye mkataba wake ulikuwa unameguka msimu huu na alikuwa huru kuzungumza na timu nyingine ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Simba.

Hivyo kwa timu ambazo zimevutiwa naye ni muda wa kukaa mezani na Simba ili kujua namna gani wanaweza kuvunja mkataba.


USAJILI WA CHIKWENDE NDANI YA AZAM FC UPO HIVI MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply