Home Azam FC AZAM FC WAPO TAYARI KWA MZUNGUKO WA PILI

AZAM FC WAPO TAYARI KWA MZUNGUKO WA PILI


 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mzunguko wa pili kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya na bado wanaendelea kuyafanya.

Azam FC ipo chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina ambaye alichukua mikoba ya Kocha Mkuu,Aristica Cioaba ambaye alifutwa kazi kwa kile ambacho walieleza kuwa timu hiyo haina mwendo mzuri.

Iliweka kambi visiwani Zanzibar na ilicheza mechi tatu za kirafiki ambapo ilishinda mechi mbili na kupoteza mechi moja.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wana amini watarejea kwenye kasi ya mwanzo.

“Wachezaji wana ari na kila mmoja amekuwa akifanya vizuri ndani ya uwanja hasa kupitia mechi za kirafiki ambazo zimetujenga na kutufanya tuzidi kuwa imara.

“Kikubwa ambacho kwa sasa tunakifikiria ni kuendelea kuwa kwenye ubora wetu na kupata matokeo chanya ambayo yatatufanya tuzidi kuwa imara,” amesema.

Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya tatu imekusanya jumla ya pointi 32.Kwenye mechi hizo za kirafiki wachezaji ambao walikuwa hawapati nafasi kikosi cha kwanza ikiwa ni pamoja na Awesu Awesu ambaye ni ingizo jipya kutoka Kagera Sugar waliweza kuonyesha makeke yao.

SOMA NA HII  RASMI...AZAM FC WAZIDI KUTIA MACHUNGU SIMBA SC...WAMALIZANA NA SOPU KWA DAU NONO...ALAMBISHWA MIAKA MITATU...